MTANGAZAJI mkongwe wa Kenya, Leonard Mambo Mbotela, amefariki dunia.
Mkwe wake, Anne Mbotela, amethibitisha habari za kicho hicho akieleza kuwa Mbotela alikuwa mgonjwa kwa muda kabla ya kuaga dunia leo.
Mbotela alijulikana kwa kipindi chake maarufu cha redio na televisheni, “Je, Huu ni Ungwana?”, kilichorusshwa hewani kupitia Shirika la Utangazaji Kenya (KBC).
Alianza kazi yake ya utangazaji mwaka 1964 katika Sauti ya Kenya, ambayo sasa ni KBC, na alitangaza kwa zaidi ya miongo mitano.
Mbotela ameacha mjane, Alice Mwikali na watoto watatu, Aida, Jimmy na George Mbotela.