BEKI wa zamani wa Manchester United, Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Raphael Varane amestaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 31.
Varane alijiunga na Como ya Italia kwa uhamisho huru mwezi Julai lakini alipata jeraha la goti mwezi uliopita katika mchezo wake wa kwanza Ligi Kuu ya Serie A dhidi ya Sampdoria.
SOMA: City, United mechi dume
Beki huyo wa kati amesema atabaki katika timu hiyo akiwa na jukumu ambalo sio la kucheza.
“Nataka kuacha soka nikiwa na nguvu. Inahitaji ujasiri mkubwa kusikiliza moyo wako na silika yako,”ameandika kwenye Instagram.