MKUTANO WA TGS: Ajenda ya uchumi wa buluu yamkosha Katibu Mkuu Kiongozi

Tukio hilo linatarajiwa kuwakutanisha wajiolojia zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya Tanzania ambapo miongoni mwa mada zitakazojadiliwa ni mchango wa tasnia ya jiolojia katika uchumi wa buluu.

ZANZIBAR KATIBU Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhandisi Zena Ahmed Said ameipongeza Jumuiya ya Wajiolojia nchini (TGS) kwa uamuzi wake kufanya mkutano wa mwaka visiwani humo sanjari na kuchagua  dhima inayochagiza uchumi wa buluu.

Mhandisi Zena ametoa pongezi hizo Mjini Unguja Ijumaa wakati alipokutana na kamati ya utendaji ya TGS kwa lengo la kujadili maandalizi ya mkutano huo uliopangwa kufanyika Novemba 7-11, mwaka huu visiwani Zanzibar.

Tukio hilo linatarajiwa kuwakutanisha wajiolojia zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya Tanzania ambapo miongoni mwa mada zitakazojadiliwa ni mchango wa tasnia ya jiolojia katika uchumi wa buluu.

“Serikali ipo tayari kushirikiana nanyi kufanikisha mkutano huu muhimu kwa kada ya wanajiosayansi. Tunatambua mchango wa wanajiosayansi katika kuchagiza uchumi wa buluu hususan katika eneo la ugunduzi wa mafuta na gesi asilia pamoja na madini yanayopatikana baharini.

“Ni matumaini yetu kuwa kupitia mkutano huo wanajiosayansi watakuja na mikakati na mapendekezo kwa Serikali juu ya namna bora ya kuendeleza rasilimali hizo,” alieleza Mhandisi Zena.

Katika kikao hicho, viongozi kadhaa wa TGS walihudhuria akiwemo Rais wa jumuiya hiyo, Dk Elisante Mshiu na Makamu wake, Dk Emmanuel Kazimoto.

Akizungumza katika kikao hicho, Dk Mshiu alieleza kuwa mkutano huo utatoa fursa kwa wajiolojia na wanajiosayansi kwa ujumla kujadili mchango wao katika kuchagiza uchumi wa buluu.

“Maandalizi ya mkutano kwa ujumla yanaendelea vizuri na tayari hatua kubwa imepigwa. Niseme kwa ufupi tu kuwa mkutano wa mwaka huu sio wa kukosa na ni fursa adhimu kwa wanajosayansi kuelewa kwa mapana dhana nzima ya uchumi wa buluu na nafasi ya kada hii katika kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya dhana hii,”ameeleza.
Katika hatua nyingine, Uongozi wa TGS ulikutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Joseph Kilangi pamoja na uongozi wa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia (ZPRA).

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Elsa J. Clark
Elsa J. Clark
2 months ago

Single Mom With 4 Kids Lost Her Job But Was Able To Stay On Top By Banking Continuously DOLLER 1500 Per Week With An Online Work She Found Over The Internet
.
.
.
Check The Details HERE_____ https://Fastinccome.blogspot.Com/

Last edited 2 months ago by Elsa J. Clark
Money
Money
2 months ago

Taulo za kike

Tangazo.PNG
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x