MOF yaendelea kuchangisha ujenzi vyoo shule ya Mwendapole

DAR ES SALAAM: Mkurugenzi wa Taasisi ya Miriam Odemba Foundation (MOF) Miriam Odemba amesisitiza Watanzania kuchangia fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa vyoo na baadhi ya miundombinu katika Shule ya Misingi Mwendapole iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

Hatua hiyo ni juhudi za taasisi hiyo katika kuiunga mkono serikali kuhakikisha wanafunzi wanapata miundombinu bora na imara ya kujisomea.

Odemba amesema lengo la taasisi yake ni kujenga vyoo 14 vipya, na kukarabati 12 kuhakikisha shule hiyo inakuwa na miondombinu bora.

“Kutuunga kwako mkono ni muhimu, kwani hakuna mchango mdogo wowote unahitajika kufanikisha hili,” amesema Miriam.

Unaweza kuchangia kwa kubonyeza: Miriam Odemba Foundation 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button