Moto waua wanafunzi 17 Kenya
KENYA : RAIS wa Kenya, William Ruto ameuagiza uongozi wa Wizara ya mambo ya ndani kuanza kufanya uchunguzi wa tukio la moto lililoteketeza maisha ya wanafunzi 17 nchini Kenya.
“Tunawaombea manusura wapone haraka,” amesema kwenye mitandao ya kijamii.“Naagiza mamlaka husika kuchunguza kwa kina tukio hili la kutisha, waliohusika watachukuliwa hatua.
“Serikali chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa inakusanya rasilimali zote muhimu kusaidia familia zilizoathiriwa.” SOMA : Moto wateketeza bweni Bukoba
Hivi sasa kundi la wachunguzi limetumwa katika Shule ya Msingi ya Hillside Endarasha kuanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo lililotokea jana usiku katika shule hiyo.
Kwa upande wake, Msemaji wa polisi Resila Onyango amesema miili imeweza kupatikana lakini imeshindwa kutambulika.
SOMA : Wanafunzi 17 wafariki kwenye mkasa wa moto katika shule ya msingi ya Hillside Endarasha Academy