Moto waua watu 100 harusini
ZAIDI ya watu 100 wamekufa na wengine 150 kujeruhiwa baada ya moto kuzuka kwenye sherehe ya harusi Mkoa wa Nineveh kaskazini mwa Iraq.
–
Wizara ya Afya inasema waliojeruhiwa vibaya wamepelekwa katika hospitali zinazohusika na majeraha ya moto; wengi wako katika “hali isiyo nzuri”.
–
Mamlaka zinasema fataki zilizotumika wakati wa sherehe huenda ndizo zilisababisha moto huo watu kadhaa wamekamatwa.
–
Taarifa zinaeleza kuwa maharusi hao wamenusurika ingawa wameungua.