Mpango Sekta ya Ustawi, Maendeleo ya Jamii 2025/2026

KATIKA mwaka 2025/26 Serikali kupitia sekta ya maendeleo ya jamii inatarajia kutekeleza jumla ya miradi tisa (9) ukiwemo mradi wa TASAF ambapo kipaumbele kitakuwa katika miradi nane (8).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila mkumbo amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo wakati akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/26.

Amesema katika Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka mitano, sekta ya ustawi na maendeleo ya jamii inajielekeza kuweka mikakati kuhusu maendeleo ya watu.

amesema utekelezaji wa miradi hiyo unalenga: Kupunguza uwepo wa mila na desturi kandamizi na zenye madhara; kuimarisha mazingira wezeshi ya uendeshaji wa Mashirikia Yasiyo ya Kiserikali nchini na kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia mikopo yenye riba nafuu na majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi.

ameeleza malengo mingine kuwa ni kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai katika kuimarisha huduma za haki jinai kwa watoto na kuendelea kuwajengea uwezo watoa huduma walio kwenye mfumo wa haki jinai; kuimarisha matunzo, ulinzi na usalama wa mtoto; kupunguza matumizi yasiyo sahihi ya teknolojia ikiwemo mitandao yanayosababisha ongezeko la mmomonyoko wa maadili katika jamii.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button