Mpogolo akabidhi utekelezaji Ilani ya CCM, aeleza mafanikio

DAR ES SALAAM: MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)imetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 100 kwa kukamilisha miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa mwaka 2020/2025.

Amesema hayo leo Juni 19,2025 wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa kipindi cha miezi sita uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini humo.

Ametaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa ndani ya wilaya kuwa ni ujenzi wa maghorofa nane ya shule za sekondari yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 8 pamoja na ujenzi wa shule ya Sekondari Kitunda Relini wenye thamani ya Sh bilioni 4.6.

SOMA ZAIDI

Mafanikio Ilala yametokana na ushirikiano – Mpogolo

Akizungumzia sekta ya afya, Mpogolo huyo wa wilaya amesema serikali imejipanga kujenga vituo vya afya kila kata huku akitolea mfano wa ujenzi wa Zahanati ya Kisasa ya Mzinga pamoja na ununuzi wa vifaa tiba na madawa.

Aidha, Mpogolo amesema katika kukuza na kuimarisha uchumi kwa Wananchi, Halmashauri ya Wilaya Ilala imeweza kutenga kiasi cha Sh bilioni 18 zitakazoanza kutolewa hivi karibuni kama mikopo isiyo na riba(mikopo ya asilimia 10).

“Uwezo wa Halmashauri yetu kwenye makusanyo umeongezeka, na kama uwezo umeimarika basi hata fedha tunazozitengakwa ajili ya miradi ya maendeleo hususan kwenye barabara tuongeze kutoka kwenye asilimia 10 kwenda asilimia 20,” amesema.

Mkutano huo maalum pia ulihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar e salaam Elihuruma Mabelya pamoja na wakuu wa Idara na vitengo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button