Mradi wa maji kunufaisha 42,000 Mtwara

KATIKA kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama Mtwara Mjini unaimarika, serikali imeanzisha mradi wa ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 500,000 eneo la Airport Manispaa ya Mtwara Mikindani utakaonufaisha watu 42,000.

Kaimu Meneja Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Jamii Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Mtwara (MTUWASA), Jane Thomas amesema utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya Sh milioni 500 unatarajia kuhudumia wananchi wa maeneo ya Mangamba, Airport, Mtawanya na Mbae Mtwara mjini.

Amesema utekelezaji mradi huo umeanza ikiwa ni mmoja wa miradi mingine ya maji ambayo imeanzishwa katika kipindi cha miaka miwili ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya Mtwara mjini kwa asilimia 95 ifikapo 2025.

“Huu mradi ni moja ya miradi ya maji ambayo imeanzishwa ndani ya kipindi cha Dr Samia Suluhu Hassan kuhakikisha upatikanaji wa maji Kwa wakazi wa Mtwara mjini, ni mmoja wa miradi ambayo itapitiwa na Mwenge wa Uhuru 2023,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button