Mradi wa maji kunufaisha wananchi 20,000 Hanang

MANYARA: SHIRIKA la WaterAid limekabidhi mradi wa uboreshaji wa huduma za miondombinu ya maji na usafi wa mazingira Wilaya ya Hanang mkoani Manyara uliogharimu Sh million 425 unatarajiwa kunufaisha wakazi wasiopungua 20,036 wilayani humo.

Akizungumza leo Agosti 1, 2024 katika hafla ya makabidhiano ya mradi huo kijiji cha Bashang na Laghanga Wilaya ya Hanang, Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika hilo, Ana Mzinga amesema kwa kushirikiana na serikali shirika linalenga kufikia watu katika maeneo mbalimbali kwa kutoa huduma hiyo pamoja na vyoo bora na mazingira salama ya usafi na usafi binafsi.

Akitoa taarifa za mradi huo, Ana Mzinga amesema Septemba 2023 walizindua utekelezaji wa mradi huo mjini Katesh katika kikao cha wadau ambapo kwa sasa wananchi wanaendelea kunufaika na mradi huo.

Advertisement

SOMA: 41,168 kunufaika mradi wa maji Arusha

Meneja Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki, Leah Kaguara, alisema WaterAid inafanya kazi kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafikiwa na huduma za maji salama, usafi wa mazingira na usafi.

Amesema shirika hilo lilizindua mkakati wake mpya wa kimataifa mwaka 2022 na programu za nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Tanzania zilitengeneza na kuzindua mikakati yao mwaka 2023.

“Lengo letu la kwanza katika mkakati huu kusaidia kupatikana kwa huduma za maji, usafi wa mazingira na usafi (WASH) ziwe endelevu inayojumuisha na salama. huduma katika eneo la Wilaya ya Hanang kwa ajili ya mabadiliko mapana huku lengo la pili likilenga kuweka kipaumbele cha WASH katika sekta ya afya ili kuboresha afya ya umma,”amesema.