Mrajis Tabora asimamishwa

Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akiwa Tabora

CHECHE za Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka zimemuunguza Mrajis Msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoani Tabora, Absolom Chaliga baada ya kusimamishwa kazi kutokana na tuhuma za kushindwa kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Barua iliyoandikwa na Dk Benson Ndiyege ambaye ni Mrajis wa Vyama vya Ushirika inasema kuwa Chaliga anasimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake. “Amesimamishwa kwa mujibu wa kanuni namba 37 ya kanuni za utumishi wa umma za Mwaka 2003,” alisema Dk Ndiyege.

Akiwa wilayani Uyui kwenye ziara yake mkoani Tabora kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, Shaka aliiomba serikali kumwondoa mrajis huyo baada ya kupata malalamiko kila wilaya aliyozuru juu ya utendaji wake wa kazi. “Changamoto za bwana huyu imekuwa donda sugu, tumetoka Kaliua analalamikiwa, tumetoka Sikonge analalamikiwa, tumetoka Urambo analalamikiwa, leo tuko Uyui watu wanalia na huyu bwana. Urasimu umekuwa mkubwa sana,” alisema Shaka.

Advertisement

Aliongeza: “Utitiri na ukiritimba umekuwa mkubwa sana kiasi unadumaza jitihada na huko tunakotoka hajasajili vyama kwa sababu kuna mawakala wanapita chini kwa chini, mbunge kasema na mimi taarifa ninazo wako mawakala wanapita chini kwa chini kuwaambia wakulima nenda kajiunge pale. Yeye sio kazi yake, yeye sio jukumu lake la nani akajiunge ushirika gani.