Mvua yatikisa Kigoma, nyumba 121 zaathirika

KIGOMA; NYUMBA 121 na makanisa manne zimeezuliwa paa, huku nyingine zikiharibika kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambapo kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu kuanza kwa mvua hizo, zaidi ya kaya 100 zimeathirika.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hashim Mvogogo, alitoa taarifa hiyo wakati akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, ambaye aliongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na Kamati ya Maafa kukabidhi misaada iliyotolewa na halmashauri kwa waathirika wa mvua hizo.

Mvogogo alisema kata zilizoathirika zaidi ni Gungu, ambako nyumba 70 zimeathirika, Kibirizi nyumba 47, Mwanga Kusini nyumba mbili na Katubuka nyumba mbili.

Alisema katika kukabiliana na hali hiyo, halmashauri imewasilisha tani 2.6 za mchele, tani 1.9 za unga wa mahindi, tani moja ya maharage pamoja na sukari, mafuta ya kupikia na sabuni za kufulia.

Aliongeza kuwa halmashauri inaendelea kushughulikia mahitaji mengine ya waathirika, ikiwamo magodoro, shuka, blanketi na maturubai, huku baadhi yao wakihifadhiwa katika maeneo mbalimbali.

Akikabidhi misaada hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, aliwataka wananchi kufuata maelekezo ya wataalamu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Serikali kwa kuchukua tahadhari dhidi ya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha nchini.

Balozi Sirro alisema tayari maeneo hatarishi yametambuliwa na wananchi wanaoishi katika maeneo hayo wameelekezwa kuhama kwa ajili ya usalama wao.

Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wakikaidi kuhama na kubeza tahadhari zinazotolewa kuhusu mvua hizo, akisisitiza kuwa Serikali itachukua hatua za kisheria dhidi ya watakaokaidi maelekezo ya mamlaka.

Pamoja na hayo, alisema Serikali itaendelea kuchukua hatua na kuwasaidia wananchi watakaoathirika na mvua hizo, akieleza kuwa Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa inayotarajiwa kupata mvua nyingi.

Alisema tangu Oktoba, wilaya za Kigoma, Buhigwe, Kakonko, Kasulu na Kibondo zimekumbwa na mvua kubwa zilizoambatana na upepo na kusababisha madhara kwa wananchi.

Baadhi ya waathirika, akiwamo Kobwa Kamana, waliishukuru Serikali kwa msaada wa vyakula walioupata, lakini wakaomba iongeze msaada wa vifaa vya ujenzi, hususan bati, ili kuwawezesha kurejea katika makazi yao.

Habari Zifananazo

13 Comments

  1. Mvua za mwezi mmoja kuathiri zaidi ya kaya 100, pamoja na kuezua paa za nyumba 121 na makanisa manne, ni hali ya kutisha kwa wakazi wa Kigoma Ujiji. Ni muhimu hatua za haraka za uokoaji na msaada wa makazi zichukuliwe kabla mvua hazijasababisha madhara zaidi.

  2. Mvua hizi zimeleta madhara makubwa Kigoma Ujiji, hasa baada ya nyumba 121 na makanisa manne kuezuliwa paa. Ni muhimu tathmini ya kina na msaada wa haraka vifike kwa kaya zaidi ya 100 zilizoathirika.

  3. Hali ni ya kusikitisha, hasa kwa nyumba 121 na makanisa manne yaliyoezuliwa paa ndani ya mwezi mmoja. Inahitajika tathmini ya haraka na msaada wa makazi pamoja na vifaa kwa kaya zaidi ya 100 zilizoathirika Kigoma Ujiji.

  4. Athari za mvua hizi ni kubwa, hasa nyumba 121 na makanisa manne yaliyopoteza paa ndani ya mwezi mmoja. Ni muhimu Manispaa ya Kigoma Ujiji kuharakisha msaada wa dharura na ukarabati kwa kaya zilizoathirika.

  5. Mvua kubwa kuathiri nyumba 121, makanisa manne na zaidi ya kaya 100 ndani ya mwezi mmoja ni hali ya kutisha kwa wakazi wa Kigoma Ujiji. Ni muhimu hatua za haraka za misaada na ujenzi wa miundombinu imara zichukuliwe kabla madhara hayajaongezeka.

  6. Hali ni ya kusikitisha kwa kaya zaidi ya 100, hasa baada ya nyumba 121 na makanisa manne kuathiriwa na mvua kubwa. Ni muhimu mamlaka kuharakisha msaada na tathmini ya maeneo hatarishi ili kuwalinda wananchi wa Kigoma Ujiji.

  7. Mvua hizi zimeleta madhara makubwa Kigoma Ujiji, hasa baada ya nyumba 121 na makanisa manne kuezuliwa paa. Ni muhimu hatua za haraka zichukuliwe kuwasaidia kaya zilizoathirika na kuimarisha maandalizi dhidi ya mvua zinazoendelea.

  8. Madhara ya mvua hizi ni makubwa, hasa nyumba 121 na makanisa manne kuezuliwa paa ndani ya mwezi mmoja. Serikali iendelee kutoa msaada wa haraka kwa kaya zaidi ya 100 zilizoathirika na kuweka mikakati ya kuzuia maafa zaidi.

  9. Madhara ya mvua hizi ni makubwa, hasa nyumba 121 na makanisa manne kuharibika ndani ya mwezi mmoja. Ni muhimu Manispaa ya Kigoma Ujiji kuharakisha msaada kwa kaya zilizoathirika na kuimarisha maandalizi kabla mvua zaidi hazijanyesha.

  10. Madhara ya mvua hizi ni makubwa, hasa nyumba 121 na makanisa manne kuathirika ndani ya mwezi mmoja. Ni muhimu hatua za haraka zichukuliwe kuwasaidia waathirika na kuimarisha maandalizi ya majanga katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.

  11. Mvua hizi zimeleta madhara makubwa, hasa baada ya nyumba 121 na makanisa manne kuharibika au kuezuliwa paa. Ni muhimu Manispaa ya Kigoma Ujiji kuharakisha msaada kwa kaya zaidi ya 100 zilizoathirika na kuimarisha tahadhari kadiri mvua zinavyoendelea.

  12. Hali ya nyumba 121 na makanisa manne kuathirika ndani ya mwezi mmoja ni ya kutisha, hasa kwa kaya zilizoachwa bila makazi salama. Ni muhimu mamlaka kuharakisha msaada wa dharura na tathmini ya maeneo hatarishi ili kupunguza madhara zaidi mvua zinapoendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button