Mrajisi aviagiza vyama vya ushirika kutumia mizani za kidijiti

Dodoma: MRAJIS wa Vyama vya Ushirika, Dk Benson Ndiege amevitaka vyama vya ushirika vya mazao nchini kuhakikisha vinatumia mizani za kidigitali katika kupima mazao ya wakulima ili kuondoa udanganyifu na kumlinda mkulima.
Kwa vyama ambavyo havitatumia mizani ya kidigitali vitachukuliwa hatua za kisheria.
Dk Ndiege ametoa maelezo hayo jana jijini Dodoma kwa wenyeviti na Wajumbe wa Bodi wa Vyama vya Ushirika vya mazao Tanzania Bara.
Alisema vyama vya ushirikia vya mazao Tanzania Bara vinapaswa kutumia mizani za kidigitali, lengo likiwa ni kuondoa udanganyifu kwenye upimaji wa mazao ya wakulima na kurahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi za makusanyo au mauzo ya mazao.

Aidha, Dk Ndiege alisema kwa vyama vya ushirika wa mazao vitakavyobainika kuwa na mizani ya kidijitali na havitumii au kuzitumia kwa matumizi tofauti na malengo yaliyokusudiwa, vitachukuliwa hatua za kisheria.

Pia aliwataka wakulima kuhakikisha mazao yao yanapimwa kwa kutumia Mizani zilizounganishwa na Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) ili kuwawezesha kupata malipo stahiki ya mazao yao.

Aidha, Dk Ndiege amevitaka vyama vyote vya ushirika wa mazao ambavyo bado havijatekeleza maelekezo ya ununuzi wa mizani za kidijitali kuhakikisha kuwa vinanunua mizani hizo kwa kufuata utaratibu wa manunuzi na Mwongozo wa Ofisi ya Mrajis kuhusu Ununuzi wa Mizani hadi kufikia Juni 31, 2026.

Tume ya Maendeleo ya Ushirika inaendelea na jitihada za kuimarisha Usimamizi wa Vyama vya Ushirika nchini ambapo kwa sasa moja ya kipaumbele kinachotiliwa mkazo ni kuratibu na kuhimiza vyama vya ushirika vya mazao, kuweka utaratibu wa ununuzi wa mizani za midijitali sambamba na matumizi sahihi ya mizani hizo.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button