Mrembo Rwanda anaswa kuendesha gari amelewa

Mrembo aliyetwaa taji la Miss Rwanda wa mwaka 2022 Divine Muheto akamatwa kwa kuendeshea gari akiwa amelewa

Polisi nchini Rwanda wamemkamata Miss Davine wa taji la taifa la urembo kwa kuendesha gari akiwa amekunywa pombe kupita kiasi” na kuharibu miundombinu.

Divine Muheto, 21 pia anatuhumiwa kwa kuendesha gari bila leseni na kutoroka eneo la ajali baada ya kugonga miundombinu, polisi walisema.

Advertisement

Muheto, 21, alipata umaarufu aliposhinda shindano la urembo la Miss Rwanda 2022, kabla ya serikali kusitisha shindano hilo kwa tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya waandaaji.