Mshindi wa mil 10/- aahidi kujenga msikiti

DAR ES SALAAM: Mshindi wa hundi ya Sh milioni 10 Umriya Omari amesema fedha hizo atazielekeza katika ujenzi wa kujenga Msikiti.

Amesema msikitini ambao alishaanza kujenga na sasa anaenda kukamilisha ujenzi wa msikiti aliouanza kupitia pesa za ushindi.

Akizungumza na habari leo baada ya kushinda Umriya Omari amesema anafurahia ushindi huo kwakuwa umekuja kwa wakati shihihi kwake.

“Nilifurahi sana kushinda. Hizi fedha nitazitumia kumalizia ujenzi wa msikiti, jambo ambalo lilikuwa linahitaji msaada mkubwa,” amesema.Umriya

Kwa upande wake Pantaleo Masawe amesema hakuwai kuamini bahati nasibu ila ametokea
mshindi wa gari aina ya Subaru Forester lenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 30, katika droo ya wateja walionunua gari katika kampuni ya Jan International Group jijini Dar es Salaam.

Mshindi huyo, Pantaleo Masawe, alisema hakuwahi kuamini kama siku moja angeweza kushinda zawadi hiyo, licha ya kupewa fomu ya kushiriki mara baada ya kununua gari lake.

“Kwa kweli niliona kama ni jambo lisilowezekana. Nilipopewa kadi ya kujaza nilichukulia kawaida tu, sikuamini kama naweza kushinda hadi nilipopigiwa simu,” amesema Pantaleo baada ya kutangazwa mshindi.

Ameongeza kuwa ushindi huo umempa imani na kuwataka wananchi kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa kwa wateja, akisisitiza kuwa hakutarajia kushinda zawadi kubwa kiasi hicho.

Mbali na mshindi wa gari, washindi wengine waliibuka na zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu, pikipiki, jokofu, televisheni, simu za mkononi, laptop pamoja na mashine ya kufulia.

Kwa upande wao, washindi wengine ni Sharif Iyanja aliyeshinda pikipiki, Haroub Seif aliyepata mashine ya kufulia, Upendo Godlove aliyeshinda laptop, Elias Edward aliyepata simu aina ya Samsung Galaxy S25, huku Shelina Suman akiondoka na televisheni aina ya Hisense ya inchi 85.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Joram Joseph, amesema droo hiyo ilisimamiwa kwa kuzingatia misingi ya haki na uwazi.

Alisisitiza kuwa washiriki na waandaaji wa promosheni wanapaswa kufuata sheria, ikiwa ni pamoja na kupata vibali na leseni stahiki pamoja na kutekeleza wajibu wa kikodi.

“Droo ilikuwa ya haki na uwazi, na aliyeshinda ameshinda kihalali. Ni muhimu kwa waandaaji kufuata masharti yote ya kisheria,” alisema.
Kwa upande wake, Meneja wa Masuala ya Kampuni, Steven Mheza, amesema

kampuni hiyo imeendelea kupata mwitikio mkubwa wa wateja tangu ilipoanza shughuli zake mwaka 2023, hali iliyochangiwa na ubora wa huduma wanazotoa.

Ameongeza kuwa wamejikita kuhakikisha wateja wanapata huduma bora kwa wakati, ikiwemo kushughulikia changamoto zinazoweza kujitokeza baada ya manunuzi.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button