Msigwa ataja maboresho maonesho ya Sabasaba

DAR ES SALAAM: MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba kwa mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo ‘Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba ni Fahari ya Tanzania’ ikilenga kuonesha thamani na nafasi ya Tanzania kama kitovu cha biashara Afrika Mashariki.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msigwa amesema lengo kuu la maonesho haya ni kutoa jukwaa kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kutangaza bidhaa na huduma zao, huku akifichua kuwa hadi sasa nchi 23 zimethibitisha ushiriki wao rasmi katika maonesho hayo.

Kwa upande wa maboresho, Msigwa amesema teknolojia imetumika kuboresha mfumo wa kutafuta na kuchukua nafasi za mabanda, kununua tiketi za kuingia, pamoja na kufanya malipo ya maegesho. Aidha, kupitia Tovuti na App ya TanTrade, sasa kuna ramani ya kidijitali itakayomsaidia mtumiaji kujua eneo analotaka kwenda katika viwanja vya maonesho.

Ameongeza kuwa kwa mwaka huu, TanTrade kwa kushirikiana na Shirika la Posta wameanzisha huduma mpya ya usafiri wa ndani ya viwanja vya maonesho pamoja na huduma ya kusafirisha mizigo ya wananchi kutoka viwanja vya Sabasaba kwenda majumbani mwao kwa gharama nafuu.

“Lengo letu ni kufanya Maonesho ya Sabasaba yawe jukwaa la kweli la biashara, ubunifu na huduma bora kwa Watanzania,” amesema @gersonmsigwa akiwa @tantradetz @posta_tz

#Sabasaba49 #FahariYaTanzania #BiasharaKimataifa #TanTrade #Msigwa #MaendeleoKazini

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button