Msigwa: Bandari haijauzwa, achaneni na wazushi

MSEMAJI Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Bandari ya Dar es Salaam haijauzwa na wanaoeneza habari hizo ni wazushi na waongo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Juni 24, 2023 Msigwa amesema kilichofanyika ni Makubaliano ya Awali ya Uwekezaji kati ya Tanzania na Serikali ya Dubai yanayolenga kuimarisha ufanisi wa bandari yanayodumu kwa miezi 12

“Hakuna bandari iliyouzwa, hakuna bandari itakayouzwa wala hakuna mpango wa kuuza bandari yoyote kwa sababu Katiba ya nchi inakataza na pia sheria za nchi zinakataza,” amesema Msigwa.

Amesema, uwezo wa bandari hiyo kwa sasa inaweza kuingiza shilingi trilioni saba kwa mwaka lakini ikiendeshwa na mwekezaji itaweza kuzalisha kiasi cha Sh trilioni zaidi ya 26.

Aliwataka wanaovumisha kuwa bandari zote zimeingizwa katika uwekezaji huo kuona aibu na kurejea katika makubaliano ili wayasome vizuri na kwamba ni Bandari ya Dar es Salaam pekee ndiyo itakayoendeshwa na mwekezaji

Amesema katika bandari hiyo sio kila kitu kitakuwa chini ya mwekezaji kwa sababu makubaliano yamelenga kuanzia gati 0 hadi gati namba saba wakati bandari hiyo ikiwa na magati 12 hivyo kuna magati Matano hayataguswa katika uwekezaji huo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button