MASHINDANO ya kusaka vipaji yajulikanayo kama Bongo Star Search (BSS), msimu wa 13 yalizinduliwa rasmi usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, muandaaji wa shindano hilo, Rita Paulsen, alisema kuwa msimu huu wa BSS utakuwa tofauti kidogo na miaka mingine.
“Mwaka huu mambo ni mengi na makubwa, msimu huu kuna mengi yamebadilika hasa katika upande wa majaji, tumejikita zaidi na wasanii,” amesema Rita.