‘Msiwazie ajira ni TRA pekee’

CHUO  cha Kodi kimewataka vijana wanaosoma chuoni hapo kuondoa dhana kuwa sehemu pekee wanayoweza kupata ajira ni Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), bali watafute fursa maeneo  mengine.

Ofisa Mkuu wa Mawasiliano wa TRA , katika chuo hicho, Oliver Njunwa amesema hayo Dar es Salaam katika maonesho ya vyuo vikuu nchini inayoendelea katika viwanja vya Mnazimmoja.

Advertisement

Amesema vijana wengi wanaofika katika banda hilo wamekuwa wakiuliza fursa za kupata ajira baada ya kuhitimu katika chuo hicho, wakiamini kuwa hakuna sehemu nyingine wanayoweza kuzipata.

“Wanafunzi wengi  wanafika hapa wakiuliza kama baada ya kuhitimu masomo wanaweza kupata ajira katika Mamlaka ya Mapato, kumbe hawajui kama masomo yatolewayo chuoni hapo yanawawezesha kwenda maeneo  mengine pia,” amesema.

Amesema chuo hicho kilianzishwa kwa malengo ya kutoa mafunzo kwa wafanyakazi, ili kuongeza weledi wa kukusanya mapato, lakini pia hutolewa kwa wadau  ili kujua kuchakata kodi katika kazi mbalimbali.

Amesema mafunzo hayo yanawezesha mwanafunzi kufanya  kazi kwa weledi kuwa kuwa zipo fursa ndani ya Tanzania na hata nje ya nchi kuhusu kodi.

Amesema mhitimu anaweza pia kuajiriwa katika mamlaka hiyo, lakini pia isiwe kwamba ili kupata kazi ni muhimu kusoma katika chuo hicho,wajue kuna fursa katika taasisi nyingine za serikali ambazo mhitimu anaweza kushauri kuhusu  masuala ya kodi.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *