PPP imeleta mapinduzi safari za kwenda Makka π

DAR ES SALAAM: MKURUGENZI wa Kituo Cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC ) David Kafulila amesema Leo ni sikukuu muhimu sana kwa Waislamu wote duniani wakati wakisherehekea sikukuu ya Eid al-Adha maarufu kama Eid ya Kuchinja.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Kafulila amesema kuwa ni kipindi ambacho kinawakutanisha Waislamu wengi duniani katika Mji wa Makka kama sehemu ya kutimiza nguzo ya 5 ya Uislamu.
Amegusia kuwa moja ya changamoto kubwa iliyokuwa ikisumbua huko nyuma ni muda mrefu ambao mahujaji walikuwa wanautumia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Abdulaziz – KAIA uliopo Jeddah.
Aidha amesema Mahujaji walikuwa wanatumia kati ya saa 6 hadi 10 kukamilisha taratibu za uwanjani miaka kabla ya mkataba wa Ubia/PPP kuendesha uwanja huo.
Ili kutatua changamoto hiyo, Serikali ya Saudi Arabia ilitekeleza mradi mkubwa wa kuboresha uwanja huo kwa kufanya upanuzi wa Hajj Terminal kupitia mkataba wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi PPP wenye thamani ya dola milioni 249 uliosainiwa mwishoni mwa mwaka 2006 na kukamilika ujenzi mwaka 2011.
Mradi huu ulijengwa kwa mkataba wa PPP wa miaka 20 kati ya Mamlaka ya Anga ya Saudia GACA na Kampuni Binafsi ya Hajj and Umrah Terminals Development Company – muungano ulioongozwa na Saudi Binladin Group kwa ushirikiano na AΓ©roports de Paris Management.
Mshauri mwelekezi wa mradi huu alikuwa shirika la kimataifa la IFC, mwanachama wa Benki ya Dunia.
Baada ya ‘Terminal’ hii kuanza kuendeshwa kwa mfumo wa PPP, ufanisi uliongezeka kwa kiwango kikubwa sana:
Ameongezea kuwa Uwezo kwa saa
Kabla ya PPP: Takriban abiria 1,000-1,500 kwa saa.
Baada ya PPP, Zaidi ya abiria 8,000 kwa saa, – ikijumuisha takriban abiria 3,800 wanaowasili na 3,500 wanaondoka kwa saa.
Amesema Uwezo kwa siku
Kabla ya PPP: Takribani abiria 25,000-30,000 kwa siku.
Baada ya PPP: Zaidi ya abiria 91,000 wanaowasili na abiria 84,000 wanaondoka kwa siku wakati wa kilele cha msimu
“Uwezo kwa mwaka:
Kabla ya PPP: Wastani wa mahujaji milioni 1 tu kwa mwaka.
Baada ya PPP: Kati ya abiria milioni 8 hadi milioni 9 kwa mwaka. – kwa mfano, ilihudumia mahujaji milioni 8.8 mwaka 2015
“Muda wa kukamilisha taratibu.
Kabla ya PPP: Abiria walitumia saa 6 hadi 10 uwanjani.
Baada ya PPP: Sasa wanatumia dakika 45 tu hadi saa 1 kukamilisha kila kitu.
“Fikiria ufanisi uliosababishwa na PPP! Muda umepungua zaidi ya mara 8 huku uwezo ukipanda mara 8-9” amesema Kafulila
Aidha mbali na kuwatakia Waislamu wote heri ya sikukuu hii muhimu ya kuchinja, Kafulila amewakuwakumbusha Watanzania kwamba PPP imesaidia pakubwa kuongeza ufanisi katika ibada ya Hijja. Hivyo basi, wasiogope kuwakaribisha wawekezaji kupitia mifumo ya PPP kwenye viwanja vya ndege hapa nchini ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na kiutendaji.
Tathmini ya usafiri wa ndege duniani mwaka 2023 ilionesha kuwa, wakati viwanja vya ndege vinavyoendeshwa kwa mfumo wa PPP ni asilimia 14% tu duniani, vilitumiwa kuhudumia takribani asilimia 40% ya abiria wote duniani.



