MSUMBIJI : TUME ya uchaguzi nchini Msumbiji inatarajiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais na bunge uliofanyika 9 Oktoba mwaka huu.
Kwa sasa hali ya wasiwasi imeongezeka nchini humo kabla ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa ambayo yanatarajiwa kutangaza ushindi wa chama tawala cha Frelimo.
Hatahivyo, Rais Filipe Nyusi amewaambia waandishi wa habari kuwa hatua ya kuchochea umma kufanya maandamano kutatengeneza mazingira ya vurugu na ni suala ambalo litaangaliwa kama uhalifu.
Naye Mgombea wa upinzani, Venancioa Mondlane, ameamua kuitisha maandamano ya siku 25 kupinga mauaji ya wakili wake Elvino Dias aliyepigwa risasi mara 25 na vikosi vya usalama nchini humo.