KOCHA Mkuu timu ya taifa “Taifa Stars’ Hemed Suleiman ametangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiandaa na michezo miwili kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON 2025) dhidi ya Ethiopia na Guinea.
Kocha Hemed amewataja wachezaji hao kuwa ni Aishi Manula, Zuber Foba, Metacha Mnata, Lusajo Mwaikenda, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Paschal Msindo, David Bryson, Ibrahim Hamad, Dickson Job, Mohamed Ame na Abdulrazack Hamza.
SOMA: Taifa Stars katika mtihani kufuzu AFCON leo
Wengine ni Adolf Mtasingwa, Novatus Dismas, Habib Khalid, Mudathir Yahya, Feisal Salum, Mbwana Samatta, Clement Mzize, Kibu Dennis, Simon Msuva, Idd Nado, Ismail Mgunda, Abdulkarim Kiswanya, Cyprian Kachwele na Nasoro Saadun.
Stars itacheza dhidi ya Ethiopia ugenini Novemba 16 kabla ya kumaliza mechi za makundi nyumbani dhidi ya Guinea Novemba 19.
Tanzania ipo nafasi ya tatu kundi H ikiwa na pointi minne baada ya michezo minne huku Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ikiongoza kwa pointi 12, ikifuatiwa na Guinea yenye pointi sita na Ethiopia ni ya mwisho kwenye msimamo ikiwa na pointi moja.