Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan amewataka vijana kutafsiri kwa vitendo maana halisi ya uhuru na mapinduzi kwa kuleta mapinduzi ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ili kutengeneza mazingira sahihi ya kuwa na maendeleo.
Akizungumza leo Januari 10,2023 kwenye Kilele cha Matembezi Maalum ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Rais Dk Samia amesema kuwa kazi ya Serikali sio kutengeneza ajira bali kuweka mazingira mazuri ya vijana kujiajiri.
“Tunalotakiwa kufanya vijana ni kutengeneza ukwasi, muwe na miradi midogo midogo, kazi ya serikali ni kufanya makusanyo makubwa na kutekeleza miradi, kazi yenu vijana ni kujitengenezea miradi ambayo itawapatieni fedha, fedha ile ndiyo itakayoleta mzunguko…
…Tumezoea katika Taifa letu suala la ukusanyaji mapato na kutafutaf edha za kuendesha mambo yetu ni suala la serikali, nilikuwa naangalia kwenye TV Watanzania walikuwa wanahojiwa kuhusu ajira, kila anayehojiwa anamalizia serikali itengeneze ajira.” amesema Rais Samia