Mtanzania ang’ara kuogelea baharini Kenya

NAIROBI: LOLITA Borega ameibuka gumzo baada ya kung’ara katika mashindano ya AA Junior and Senior Open Water Swimming Championship yaliyofanyika Nyali Beach, Mombasa – Kenya.

Borega aliweka rekodi mbili muhimu – kuwa mchezaji mdogo zaidi na mwanamke wa kwanza kutoka Tanzania kushiriki rasmi mashindano ya aina hiyo.

Alionesha uwezo mkubwa kwa kuogelea km 1.5 kwa muda wa dakika 29:54, na kufuzu hatua ya Nusu Fainali ya mbio za  km 3, ambako alitumia dakika 18:24, na kuipa Tanzania pointi 4 na nafasi ya saba kati ya timu tisa.

Kwa upande wa wanaume, Rajab Khamisi  aliogelea dakika 29:38, na Kabeer Lakhani dakika 31:47, wakimaliza kwa heshima licha ya kukosa Nusu Fainali.

Meneja wa timu, Ramadhan Namkoveka, alisema ushiriki huo wa kihistoria umekuwa darasa muhimu kwa Tanzania kuelewa kiwango cha kimataifa.

“Ushiriki huu umetupa mwanga wa mwelekeo wa timu yetu katika kuogelea baharini,” alisema Namkoveka, akibainisha kuwa timu sasa inajiandaa kwa mashindano yajayo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button