Mtoto Georgina aketi kiti cha Rais Samia

RAIS Samia  Suluhu Hassan amempisha mtoto mwenye umri wa miaka minane, Georgina Magesa na kumruhusu akae kwenye kiti chake.

Rais alifikia hatua hiyo baada ya kuona Makala fupi yam toto uyo iliyorushwa na Azam akielezea ndoto zake za kutamani kuwa Rais wa Tanzania siku moja.

“Ni katoto…kajukuu ka kiafrika…ambako kana mtazamo wa mbele na mtazamo mkubwa. Kameanza kazi ya kuandika vitabu kwa umri ule…Mungu amkuze…Mungu amnyooshee afike pale anapotaka…” Rais Samia akitoa baraka kwa mtoto Georgina Magesa, mwenye ndoto za kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia amekutana na mtoto huyo leo Mei 18,2023 kwenye  uzinduzi wa minara ya mfumo wa urushaji wa matangazo ya televisheni ya Azam Media Limited kwa kutumia antenna (DTT).

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button