Mtwara washerehekea kuzaliwa Rais Samia

KATIKA kuadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Mtwara ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Kanali Ahmed Abbas leo wamefanya sherehe kwa ajili kumpongeza na kumuombea Rais Samia.

Sherehe hizo zimefanyika leo katika viwanja vya Mashujaa Mjini Mtwara, ambapo tukio hilo limehudhuriwa na wanafunzi wa kike kutoka shule za msingi mkoani humu pamoja na wamama wajane.

Katika tukio hilo mashirika mbalimbali na wadau wa maendeleo katika sekta ya elimu wakimo Weatworth, walitoa zawadi za taulo za kike kwa wanafunzi kumuunga mkono Raisi Samia katika kumuwezesha mtoto wa kike kupata elimu akiwa kwenye mazingira mazuri.

Kanali Abbas alisema Raisi Samia anafanya kazi kubwa ya kulipambania taifa katika kuleta maendeleo kupitia nyanja mbalimbali za kiuchumi, na kwamba sherehe za kumbukumbu yake ya Kuzaliwa ni kumtia moyo katika utendaji wake kwa taifa.

“Ndiyo maana leo tumekutana hapa kulipa fadhila ndogo kwa kukata keki kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake,” amesema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x