JAMII mkoani Mtwara imehimizwa kuzingatia suala la elimu jumuishi na badala yake iondokane na mila na desturi ambazo haziwakubali watoto wenye mahitaji maalumu katika kupata elimu kama haki yao ya msingi.
Hayo yamesemwa wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani humo kuhusu kuwajengea uelewa ili waweze kuuelewa mkakati wa Taifa wa elimu jumuishi ili baada ya hapo waweze kuhabarisha umma kuhusiana na suala zima la mkakati huo.
Ofisa mradi wa ‘Sauti Zetu’ kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na masuala mbalimbali ya kijamii wilayani mtwara (MTWANGONET), Deogratius Makoti anasema kwa sasa serikali ina mifumo na miongozo inayosimamia watoto wote wenye mahitaji maalum kuhakikisha wanapata elimu pale walipo kulinganga na mahitaji yao.
‘’Changamoto kwetu sisi jamii sasa hatuna uelewa wa huo makakati wenyewe kwanza unasema nini… kuhusu elimu jumuishi lakini bado tuna mila na desturi ambazo haziwakubali watoto wenye mahitaji maalum, kwahiyo tukasema sasa tukutane na waandishi wa habari’’
“Lengo tuwajengee uelewa waandishi wa habari kwanza kuhusu mkakati wa taifa wa elimu jumuishi ili baada ya hapa muweze kuhabarisha umma kikamilifu kuhusu umuhimu wa elimu na ipate taarifa kuwa serikali ina mifumo rasmi na miongozo ya kusimamia na kuboresha elimu jumuishi kuhakikisha kila mtanzania kwa mahitaji aliyokuwa nayo anapata elimu’’amesema Makoti
Amesema, watoto hao wenye mahitaji maalu mara nyingi wamekuwa wakisahaulika kupata haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na haki ya kupata elimu.
Hata hivyo ameiomba jamii hiyo wasiwafiche watoto na badala yake wawapeleke shuleni ili waweze kupata elimu kwasababu elimu ni haki ya kila binadamu huku akiiomba serikali kuendelea kuajiari walimu wenye elimu maalumu kutokana na uhitaji mkubwa uliyopo mashuleni kwa sasa, mkakati ambao ulinza mwaka 2022/2026 kuhusu utekelezaji wa elimu hiyo jumuishi
Naye Mwandishi wa Habari kutoka Safari FM Radio mkoani humo, Sospeter Magumba ‘’Sisi kama waandishi tumepewa uelewa na tumeelewa vizuri kwahiyo kazi iliyopo mbele yetu ni kwenda kutoa taarifa, kufanya ushawishi na utetezi kwa jamii ili iweze kuelewa haya masuala ya mahitaji maalum’’