Mtwara yatenga hekta 16,600 za umwagiliaji

MTWARA — Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, amesema kuwa Mkoa wa Mtwara una jumla ya hekta 16,644 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, ingawa ni hekta 3,848.6 tu ndizo zinazomwagiliwa kwa sasa.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Tunza Issa Malapo, Naibu Waziri Silinde amesema kuwa kati ya eneo linalomwagiliwa, hekta 1,337.8 zinatumia miundombinu ya kisasa ya umwagiliaji iliyoendelezwa na Serikali, huku hekta 2,510.8 zikitegemea mifereji ya asili.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Mtwara una jumla ya hekta 1,421,200 zinazotumika kwa kilimo kwa ujumla, hivyo Serikali inaendelea na jitihada za kuongeza maeneo yanayomwagiliwa ili kuongeza uzalishaji na tija kwa wakulima wa mkoa huo.
SOMA PIA: