UINGEREZA : RAIA wa Uingereza amegundulika ana virusi vya ugonjwa wa homa ya nyani maarufu “Mpox”
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Uingereza kutangaza mlipuko wa ugonjwa wa Mpox ambapo awali ugonjwa huu ulitangazwa kama ugonjwa wa hatari katika baadhi ya maeneo ya Afrika.
Wataalamu wa afya wamesema ugonjwa wa Mpox ni sehemu ya mlipuko wa virusi vya Clade 1b, ambao unasambaa kwa urahisi na haraka kupitia maambukizi ya mtu mmoja kwenda mtu mwingine.
Taarifa za awali zimesema Raia huyo wa Uingereza alikuwa likizoni katika moja ya nchi za Afrika ambapo alianza kuumwa tangu akiwa safarini kurejea Uingereza na alipofika hali ikabadilika.