Museven akutwa na maambukizi ya corona

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amepimwa na kukutwa na COVID-19, yuko katika afya njema na ataendelea na majukumu yake, huku akipata matibabu, Ofisa Mkuu Wizara ya Afya amesema jana.

“Leo …(jana) Rais amepimwa na kukutwa na COVID-19. Hii ilikuwa baada ya kupata dalili kama za mafua. Hata hivyo yuko katika hali nzuri na anaendelea kutekeleza majukumu yake kama kawaida huku akizingatia SOPs,” Diane Atwine, Katibu Mkuu Wizara ya Afya alisema.

Mapema jana baada ya kutoa hotuba ya taifa katika viwanja vya Bunge, Museveni, 78, alitoa dokezo la kwanza kwamba huenda alikuwa ameambukizwa COVID, akisema asubuhi alihisi baridi kidogo, na kumfanya aombe vipimo.

Alisema vipimo viwili kati ya vitatu alivyofanya vilikuwa hasi, na alikuwa akisubiri matokeo ya mwingine.

“Kwa hiyo mimi ni muathirika wa corona na nimesimama hapa. Ndio maana umeniona nikija kwa magari tofauti na Mama,” Museveni alisema.

Habari Zifananazo

Back to top button