Musk abadili mfumo kuona tweets

MMILIKI wa Twitter, Elon Musk ametangaza mfumo mpya wa matumizi ya mtandao huo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Musk ametoa taarifa kuwa watumiaji wenye ‘Blue Tick’ wanaweza kuona tweets 6,000 kwa siku.

pharmacy

Aidha, watumiaji wasio na uthibitisho wa ‘Blue Tick’ watakuwa na uwezi wa kuona tweets 600 pekee kwa siku.

Musk ameeleza kwa watumiaji wapya wa mtandao huo ambao pia hawajathibitishwa na mfumo huo watakuwa na uwezo wa kuona Tweets 300 tu.

Tajiri huyo ameeleza sababu za mabadiliko hayo ni kushughulikia viwango vilivyokithiri vya uchakachuaji wa data na upotoshaji wa mfumo wa mtandao huo.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button