Musk amwita Zuckerberg kuku
UGOMVI unaoendelea kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Meta, Mark Zuckerberg na Mkurugenzi wa SpaceX, Elon Musk umechukua sura mpya baada ya Musk kumdhihaki Zuckerberg kwa kumwita kuku.
Hayo yanajiri baada ya Zuckerberg kutangaza kutofanyika pambano lao akiamini Musk hachukulii kwa ukubwa
Awali akizungumzia pambano hilo Zuckerberg alisema: “Nadhani sote tunaweza kukubaliana kwamba Elon hayuko makini na ni wakati wa kuendelea na mengine. Nilitoa tarehe halisi,” aliandika Zuckerberg kwenye Threads.
“Elon hajathibitisha tarehe, halafu anasema anataka kufanyiwa upasuaji, nakwenda kushindana na watu ambao wanachukulia michezo kwa ukubwa.
” Aliongeza.