Muswada huduma za habari wasogezwa mbele

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Serikali imesogeze mbele uwasilishaji wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ambao ulipangwa kuwasilishwa katika Bunge linaloendelea ikiwa ni sehemu ya miswada ya mabadiliko ya sheria mbalimbali.

Kwa taarifa hiyo, muswada huo sasa utawasilishwa katika Bunge la Bajeti linalotarajiwa kuanza mwezi Aprili mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma, Leo Februari 7, Msigwa amesema muswada huo unatarajiwa kufanyia mabadiliko ya Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016.

Advertisement

“Jambo letu tulikuwa tumepanga tuliwasilishe lakini ndugu zangu imetokea kwamba ratiba ya bunge imebana sana, hakukupatikana nafasi, kwahiyo tumeshindwa kuwasilisha muswada wa mabadiliko ya sheria hii ya habari.” amesema Msigwa.

Msigwa amesema zipo sheria nyingi ambazo hazikupata nafasi ya kuwasilishwa na kujadiliwa bungeni hata hivyo ameongeza kuwa katika mkutano ujao sheria hizo zitawasilishwa, kujadiliwa na kuanza kutumika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *