Muuza utumbo amuua mwenye tatizo la afya ya akili

MOROGORO: POLISI Mkoani Morogoro inamsaka mtu mmoja ambaye jina lake halijatajwa kwa tuhumza za mauaji ya Haubi Abdu Ndomi (38), ambaye ana tatizo la afya ya akili mkazi wa Mjimwema , Manispaa ya Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogor, Alex Mkama amethibitisha kutokea tukio hilo jioni ya Novemba 26, mwaka huu na kwamba cha kifo kimetokana na ugomvi baina yao, ndipo mtuhumiwa alimpochoma kisu mwenzake na kusababisha mauti.

Kamanda huyo amesema kwa vile mtuhumiwa ambaye inaelezwa anafanya biashara ya utumbo wa nyama anajulikana mtaani watamtafuta na atakapopatikana atakabiliana na mkono wa sheria.

Kwa upande wake mama wa marehemu, Hawa Iddy amesema haelewi nini kilitokea hadi muuza nyama ya utumbo kufikia kumchoma kisu mwanawe, kwani awalio walionekana kuwa na ugomvi na hata alipotoa kisu ilikuwa kama utani kumbe alidhamiria.

“Kumbe ni kweli alidhamiria akamchoma kwenye moyo …kijana wangu alisimama kama dakika mbili, akayumba na kuangua chini akitoka damu nyingi na nilipata mshangao na sikuweza kupata msaada muda huo, kwani kijana aliyetenda jambo hilo alikimbia,” amedai.

Awali, Mwenyekiti wa mtaa wa Mjimwema, Said Kolongo alisema akiwa shambani jana, alipata taarifa ya tukio hilo la mauaji ya kijana wa mtaani hapo ambaye ana matatizo ya afya ya akili.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button