Mv Mwanza kukabidhiwa Agosti

UJENZI wa meli mpya ya Mv Mwanza ‘Hapa Kazi Tu’ utakamilika mwezi Agosti mwaka huu na kukabidhiwa kwa serikali.

Meli hiyo ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 84 hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi bilioni 111.

Akitoa taarifa ya  utekelezaji wa mradi huo kwa Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 14, 2023, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL), Eric Hamisi amesema tayari serikali imelipa zaidi ya Shilingi bilioni 41 sawa na asilimia 31 ya malipo yote kwa mkandarasi Kampuni ya Gas Entec Cooperation inayotekeleza mradi huo kwa kushirikiana na Gangnam Cooperation na Suma JKT.

Amesema  meli hiyo itakapokamilika itakuwa na uwezo wa  kubeba abiria 1, 200, tani 400 za mizigo na magari 20.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x