NAIROBI: Takriban watu 15 wamekufa nchini Kenya kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha maeneo mbalimbali Afrika Mashariki.
Mvua hiyo imesababisha madhara ikiwemo kukata barabara, kusomba nyumba na kuua mifugo, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limetangaza Jumatatu.
“Kufikia jana (Jumapili), kaya 15,264 zimeathiriwa, huku 15 wakiripotiwa kuaga dunia na vifo vya mifugo 1,067”, liliandika Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya kwenye mtandao wa X.
Msimu wa mvua kuanzia Oktoba hadi Disemba katika Pembe ya Afrika unakuzwa mwaka huu na El Niño, jambo ambalo limesababisha mabadiliko ya la hali ya hewa kwa ujumla linalohusishwa na kupanda kwa joto, ukame katika baadhi ya maeneo ya dunia na mvua kubwa katika maeneo mengine.