Mwalimu afa kwa kuchomwa kisu darasani

MWALIMU wa Shule ya msingi Igaka, Kata ya Isulabutundwe, Tarafa ya Kasamwa wilayani Geita Emmanuel Chacha (35) amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu na mwalimu mwenzake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha taarifa hiyo leo na kueleza tukio lilitokea Machi 15, 2023 majira ya saa  tatu asubuhi.

Kamanda Jongo amesema marehemu alifariki baada ya kuchomwa na kisu tumboni kwenye eneo la chembe ya moyo.

“Mtuhumiwa naye ni mwalimu, mwanaume mwenye umri wa miaka 35, (jina linahifadhiwa) naye ni mkazi wa kijiji cha Igaka Kata ya Isulwabutundwe, Tarafa ya Kasamwa.

“Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea, mtuhumiwa amekamatwa, amehojiwa na amekiri kufanya tukio hilo,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button