ALIYEKUWA mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Songea Mjini mwaka 2015 na Mwenyekiti Mwanzilishi wa Kanda ya Kusini, Joseph Lusius Fuime amejiunga na ACT Wazalendo.
Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 2, 2024 na Naibu Katibu Mwenezi ACT Wazalendo, Shangwe Ayo.
SOMA: ACT Wazalendo waivuruga Chadema Lindi
Taarifa ya Shangwe imeeleza kuwa Fuime amepokewa na Kiongozi wa chama hicho, Doroth Semu mbele ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Gradon Viral Songea Mjini Ruvuma.
Katika taarifa yake Shangwe imesema kuwa kiongozi huyo ametaja rushwa kuwa ni moja ya sababu iliyomfanya kuondoka Chadema.