MwanaFA apongeza udhamini wa benki michezoni

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Hamis Mwinjuma ameipongeza Benki ya NBC kutokana na jitihada zake za kusaidia maendeleo ya michezo mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mchezo wa gofu wa NBC Lugalo Open 2023 iliyofanyika katika viwanja vya Jeshi Lugalo jana, Mh. Mwinyijuma alisema NBC imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika sekta michezo hapa nchini na kuongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa benki hiyo.

“Nikiwa kama Naibu Waziri mwenye dhamana ya Utamaduni, Sanaa na Michezo napenda kuishukuru benki ya NBC kwa kutuunga mkono katika jitihada za kuendeleza na kukuza maendeleo ya michezo.

NBC imekuwa ikifadhili michezo mbali mbali kiwa ni pamoja na ligi ya Kuu ya Tanzania bara na Dodoma Marathon. Ligi yetu kwa sasa ni moja ya ligi zinazotajwa kuwa ni ligi  bora barani Afrika na hii imewezekana kutokana  na mchango wabenki ya NBC,” alisema Mwinjuma.

Aliongeza: “Ni rai yangu kwa NBC kuendeleza kuweka mkono kwenye michezo yetu na kwenye sehemu nyingine za kijamii hapa nchini. Makampuni na taasisi nyingine pia ziige wanachokifanya benki ya NBC ili tuweze kupiga hatua kubwa na kwa haraka zaidi.”

Naibu Waziri aliipongeza NBC kufadhili michezo mbalimbali. “Sikutegemea kuwakuta kwenye gofu, nimefurahishwa na jitihada zenu kwa kuwa mstari wa mbele katika kukuza na kuimarisha michezo Tanzania. Hongereni sana NBC nyinyi ni mfano wa kuigwa,” aliongeza Mwinjuma.

Aidha, Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa benki hiyo, James Meitaron alisema kuwa kupitia sera ya kurudisha kwa jamii, benki hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kuendeleza na kukuza michezo mbali mbali nchini.

“Tunaamini kuwa ushiriki wetu kwenye eneo hili la michezo pamoja na kusaidia juhudi za serikali katka maeneneo mengine, utasaidia kuboresha maisha ya Wanzania ikiwa pia ni sehemu yetu ya kurudisha kwa jamii,” alisema.

Kama tulivyoahidi hapo awali, leo tumetoa tuzo mbali mbali kwa washiriki wa mashindano haya ya wazi ya NBC Lugalo 2023 yaliyoanza jana,” alisema Meitaron.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button