Mwanafunzi asimulia alivyokatishwa ndoto zake

MWANAFUNZI Msonge Mjuta (15) anayeishi kitongoji cha Kigoma kijiji cha Nuja kata ya Ngogwa  Manispaa ya Kahama anasimulia anasema jina hilo sio halisi na kwa masikitiko anaelezea jinsi alivyokatishwa ndoto yake

Msichana huyo aliyekuwa akisoma darasa la sita anasema kitendo cha kubakwa kimemkosesha furaha na kutimiza ndoto zake alitamani kuwa shuleni nakufikia malengo ya kuwa muuguzi.

Msichana huyo  mwaka huu alitakiwa awe darasa la saba nakutarajia kufanya mtihani wa kumaliza mwezi Septemba mwaka  huu kama wanafunzi wengine.

Anasema anaishi na bibi yake katika kitongoji hicho, Oktoba mwaka jana  bibi yake aliondoka na kwenda msibani kijiji jirani  nyumbani hapo alibaki yeye na wadogo zake wawili.

Msichana huyo anasema alikuja kijana mmoja nyumbani hapo  kuomba maji ya kunywa lakini lengo lake lilikuwa sio hilo akaingia ndani hajafika kwenye  ndoo ya maji ghafla akamshika kwa nguvu nakumuingiza chumbani kwa bibi yake  na kumfunika mtandio usoni na kumvua nguo na kumuingilia kimwili.

“Nilipiga kelele lakini aliniziba na mtandio na wadogo zangu wawili mmoja anamiaka mitano na mwingine saba wakishuhudia nakushindwa kutoa msaada  mpaka akamaliza na kukimbia…..”anasema msichana huyo.

Msichana anaeleza aliogopa kumueleza bibi yake aliporudi kutoka msibani baada ya miezi kadhaa akaanza kuona hali ya kuugua na kuwa mtoro shuleni.

“Lakini mimi niko tayari kurudi  shuleni …… napenda kusoma kwani malengo yangu badaye kuwa muuguzi”anasema msichana huyo.

Bibi wa msichana huyo anasema  hakugundua kama ni mjamzito  kwani hata kitendo cha kubakwa hakumueleza mpaka walimu walivyouita  shuleni kumueleza ana ujauzito wa miezi mitatu.

“Nilimuhoji mwijukuu wangu mimba hiyo ya nani? akaanza kunieleza ujio wa kijana huyo hapo nyumbani naona alishindwa kunieleza kwa hofu ya kumuadhibu imebidi anyamaze tuanze kumtafuta kijana huyo anaishi nyumba ya jirani.”anasema bibi.

Bibi anasema tayari amejifungua na mtoto ana miezi mitatu sasa wako tayari kumlea ikiwa msichana amekubali kurudi shuleni.

Mjomba anasema baada ya kuelezwa  kuwa ni mjamzito na shule kufukuzwa ilibidi waende kwenye familia ya kijana  aliyefanya kitendo cha kubaka  na kushtaki ambapo baba wa kijana huyo alikana kuwa mwanaye hawezi kufanya kitendo hicho.

“Baada ya kuchukua uamuzi wa kwenda  kituo cha polisi  alianza kusakwa lakini hakupatikana na baadaye kesi ilienda hivyohivyo  mahakamani tulishirikiana na walimu lakini kijana huyo alitoroshwa na wazazi wake kwa lengo la kuepuka mkono wa sheria.”anasema mjomba.

“Wanamshukuru hakimu ambaye alikuwa akisimamia kesi hiyo baba wa kijana huyo naye amehukumiwa  kifungo na kijana wake amehukumiwa miaka 12 na kuchapwa viboko 12.” anasema Mjomba.

Katika hali ya kurejea shuleni  msichana huyo anaonekana kuwa na utayari  wa kusoma  na bibi yake  wamekubalina kumuangalia mtoto huyo  akiwa nyumbani hapo.

Mjomba anasema  aliongea na walimu wa shule hiyo  kuhusu kurudi shuleni msichana amesema muongozo wa serikali unaruhusu hivyo wao wako tayari kulea mtoto arudi shule.

Mwalimu mkuu  wa shule ya msingi Nuja Ramadhani Mhoja anasema  mwanafunzi huyo kweli alifanyiwa kitendo cha ubakwaji  na mwaka huu hawezi kufanya mtihani sababu jina lake halijasajiliwa.

Hivi sasa kuna wanafunzi 52 wa darasa la saba  wasichana 23 na wavulana 29 na wanafunzi wengi wamekuwa wakiacha shule kwa utoro wa rejareja na wengine wazazi kuhama kwani mwaka jana tukio la mimba lilikuwa hilo  moja.

“ Pia mwaka juzi tukio la mimba  hapa shuleni lilikuwa moja na wazazi walishindwa kutoa ushirikiano wakutosha mtuhumiwa alikimbia na mwanafunzi hakuendelea tena kusoma.”anasema mwalimu Mhoja.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nuja Joseph Machibya  anasema taarifa ya kutaka kurudi shule kwa mwanafunzi huyo hana ila akitaka kurejea ruksa sababu tatizo alilolipata nila kikatili ambalo hakutarajia.

Ofisa elimu taaluma  msingi Manispaa ya Kahama  Maximil Zacharia  anasema msichana anapopata tatizo akiwa bado shuleni  waraka wa elimu unamtambua arudi shuleni na taarifa zitoke kwa mwalimu wa shule husika kwa maandishi.

“Changamoto ya mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi hakuna  wapo ambao wanautoro wa rejareja na wao wanaangaliwa ndipo ruhusa ya kurudia inatolewa.”anasema Zacharia.

Ofisa elimu mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako anasema  wanafunzi  wa shule ya msingi waliopata mimba ni 28 kwa mwaka 2022 na baadhi yao kesi zilikuwa zikiendelea mahakamani na kutolewa hukumu zingine  zikiendelea na upelelezi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa naibu waziri  wa Elimu,sayansi na  na Teknolojia Omary Kipanga anasema  kuna   wanafunzi  1,554 waliopata ujauzito  hapa nchini katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2022.

Kipanga anasema  kwa upande wa elimu ya msingi serikali inaendelea kukusanya taarifa za wanafunzi waliorejea shuleni baada ya kukatiza masomo kwa sababu ya ujauzito.

Waraka wa elimu namba 02 wa mwaka 2021  kuhusu  urejeshwa shuleni wa wanafunzi  waliokatiza masomo katika elimu ya msingi  na seondari kwa sababu mbalimbali.

Waraka huo unaeleza  dira ya elimu ya Tanzania  ni kuwa na Mtanzania aliyeelimika  na mwenye maarifa,  stadi, umahiri, uwezo na mitazamo  chanya  ili kuweza kuchangia  katika kuleta maendeleo  ya Taifa.

Urejeshaji shuleni  wa wanafunzi  waliokatiza masomo  ni kutokana  na sababu mbalimbali ambazo zinatokana na changamoto  za kifamilia au wazazi  kuhama  maeneo bila kufuata utaratibu  za uhamisho wa watoto wao ikiwemo kupata ujauzito.

Ili kuhakikisha watoto wote wanaendelea kupata fursa ya  kupata elimu  kama haki yao ya msingi  kupitia waraka huu serikali inatoa fursa  kurejea  katika mfumo rasmi wa elimu.

Mratibu wa Mfuko wa wanawake Tanzania  WFT-T kwa mkoa wa Shinyanga  Gloria Mbia anasema  mwanafunzi kama yuko tayari kurudi shuleni kwa hiari yake ni sawa lengo atimize malengo yake kama waraka unavyoeleza.

Kwa mujibu wa  taarifa ya  makosa ya ukatili  wa kijinsia  na unyanyasaji  kutoka jeshi la polisi nchini  wameeleza ukatili wa watoto kubakwa  kuanzia  Januari  hadi Disemba 2022 kulikuwa na  matukio 6,335 na mimba za utotoni matukio 1,555.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
juliya
juliya
22 days ago

I make about $25,000-30,000 a month online. It was enough to comfortably replace the income from my old job, especially since I only worked about 10-13 hours a week from home. I was amazed at how easy it was after trying it out, copy it under the website…
Click HERE…………. http://www.Smartwork1.com

Tibirizi, CHAKECHAKE Pemba
Tibirizi, CHAKECHAKE Pemba
21 days ago

Maoni: Draft National BANDARI Policy 2002
 
ENEO
MAONI
1.
1.2.1.2 BANDARI Resources development
Sera ya Taifa ya BANDARI imekuja wakati mzuri ambapo Dunia nzima inafikiria maendeleo endelevu (sustainable economic development) ambayo kuwa hakika yanajumuisha matakwa ya watu wengi waliopo na vizazi vijavyo. Inashauriwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na masuala mengine ya kijamii ni vyema katika mipango ya upatikanaji wa maji salama kuwepo mpango wa kuwapa ruzuku Kampuni Binafsi zinazotafuta na kuchimba visima ili wananchi/kampuni za BANDARI zinazotoa huduma BANDARI ziweze kupata huduma za maji kirahisi (surface and groundBANDARI development)
                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                        
2.
3.2.3 WasteBANDARI Quality
Kumekuwa na ukuaji wa haraka wa miji iliyopimwa na isiyopimwa mijini na vijijini kulingana na hali hiyo kumekuwa na ongezeko kubwa la uhitaji wa huduma ya Maji Taka. Licha ya kuwa na mfumo uliopo ni mzuri unaohujumuisha magari ya Majitaka. Inashauriwa katika kipengele hiki kuwepo na mpango mzuri wa fidia kwa wananchi endapo Serikali ikiamua kusimika mfumo wa jamii wa majitaka kwenye mipango miji na maeneo ya BANDARI itakayorahisisha recycling and reuse of wasteBANDARI.
3.
3.1.8 BANDARI for Socio-Economic Development
Sera ya BANDARI imeweka msukumo mkubwa katika uvunaji wa maji ya mvua ambayo yamekuwa ni hazina kubwa kwa taifa pamoja na changamoto zilizopo za kimfumo za uvunaji maji Inasharuriwa mpango wa kuendeleza mabwawa yaliyopo nchini uandaliwe kwa kuongeza ukubwa ili yaweze kuhifadhi maji (promote rainBANDARI harvesting) mengi kwa wakati mmoja na jamii ya watanzania kuweza kuyatumia katika masuala ya Utalii, Kilimo na Uvuvi.

Capture.JPG
Tibirizi, CHAKECHAKE Pemba
Tibirizi, CHAKECHAKE Pemba
21 days ago

Maoni: Draft National BANDARI Policy 2002
 
ENEO
MAONI
1.
1.2.1.2 BANDARI Resources development
Sera ya Taifa ya BANDARI imekuja wakati mzuri ambapo Dunia nzima inafikiria maendeleo endelevu (sustainable economic development) ambayo kuwa hakika yanajumuisha matakwa ya watu wengi waliopo na vizazi vijavyo. Inashauriwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na masuala mengine ya kijamii ni vyema katika mipango ya upatikanaji wa maji salama kuwepo mpango wa kuwapa ruzuku Kampuni Binafsi zinazotafuta na kuchimba visima ili wananchi/kampuni za BANDARI zinazotoa huduma BANDARI ziweze kupata huduma za maji kirahisi (surface and groundBANDARI development)
                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                        
2.
3.2.3 WasteBANDARI Quality
Kumekuwa na ukuaji wa haraka wa miji iliyopimwa na isiyopimwa mijini na vijijini kulingana na hali hiyo kumekuwa na ongezeko kubwa la uhitaji wa huduma ya Maji Taka. Licha ya kuwa na mfumo uliopo ni mzuri unaohujumuisha magari ya Majitaka. Inashauriwa katika kipengele hiki kuwepo na mpango mzuri wa fidia kwa wananchi endapo Serikali ikiamua kusimika mfumo wa jamii wa majitaka kwenye mipango miji na maeneo ya BANDARI itakayorahisisha recycling and reuse of wasteBANDARI.
3.
3.1.8 BANDARI for Socio-Economic Development
Sera ya BANDARI imeweka msukumo mkubwa katika uvunaji wa maji ya mvua ambayo yamekuwa ni hazina kubwa kwa taifa pamoja na changamoto zilizopo za kimfumo za uvunaji maji Inasharuriwa mpango wa kuendeleza mabwawa yaliyopo nchini uandaliwe kwa kuongeza ukubwa ili yaweze kuhifadhi maji (promote rainBANDARI harvesting) mengi kwa wakati mmoja na jamii ya watanzania kuweza kuyatumia katika masuala ya Utalii, Kilimo na Uvuvi….

Capture-1693377332.7122-215x300.jpg
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x