URUSI : MWANAHARAKATI Ildar Dadin ambaye alifungwa gerezani nchini Urusi kwa kuupinga utawala wa Rais Vladimir Putin, ameuawa katika uwanja wa vita wakati akipigana na vikosi vya Ukraine.
Kifo chake kimethibitishwa na vyombo vya habari vya Urusi na familia yake jana Jumapili.
Dadin amesifiwa kama “mpiganaji jasiri na aliyejitolea kimasomaso” kupambana na Putin.
Mwanaharakati huyo mwenye umri wa miaka 42 alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu gerezani mnamo mwaka 2015 kwa kuandaa maandamano dhidi ya mamlaka nchini Urusi.
SOMA : Urusi yajipanga kudungua drone za Ukraine
Dadin alikuwa raia wa kwanza wa Urusi kuhukumiwa chini ya sheria ya mwaka 2014 inayozuia maandamano nchini humo.