UINGEREZA : MWANAMFALME wa Uingereza, William Arthur Philip ameanza ziara nchini Afrika Kusini itakayojumuisha mikutano na wanaharakati wa masuala ya mazingira na utoaji tuzo ya Earthshot aliyoianzisha miaka kadhaa iliyopita.
Akiwa nchini Afrika ya kusini atafanya mazungumzo na wanaharakati na wavuvi na kutoa tuzo itakayoaambatana na kitita cha dola milioni 1.2 kwa taasisi tano zenye mawazo ya kimapinduzi katika masuala ya mazingira.
Pia ataangalia masuala ya uhifadhi wa wanyamapori unaosimamiwa na mamlaka za uhifadhi wa wanyamapori .
Mara ya mwisho alitembelea Afrika mwaka 2018 lakini kwa sasa amepanga kuwa karibu na bara la Afrika.
SOMA: Fahamu mapito ya Prince William