MAREKANI : MWANAMUZIKI na mtayarishaji wa muziki Quicy Jones amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.
Kwa mujibu wa msemaji mkuu wa mwanamuziki huyo , Arnold Robinson amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, “alifariki dunia usiku wa kuamkia jumapili nyumbani kwake Bel Air”.Amesema.
Jones alijulikana zaidi kama mtayarishaji wa albamu ya Michael Jackson ya Thriller na pia alishawahi kufanya kazi na mwanamuziki Frank Sinatra na wasanii wengine nchini Marekani.
Zaidi ya miaka 75, Jones alishinda tuzo 28 za Grammy na alitajwa kuwa mmoja wa wanamuziki wa jazz wenye ushawishi mkubwa wa karne ya 20.
Katika filamu ya The Wiz, Jones alifanya kazi pamoja na Michael Jackson mwenye umri wa miaka 19 wakati huo.
Jones pia aliendelea kutoa albamu ya Jackson Off the Wall ambayo iliuza nakala milioni 20.
Mnamo 1985, Jones alikusanya waimbaji 46 maarufu wa Marekani wakiwemo Jackson, Bruce Springsteen, Tina Turner na Cyndi Lauper na kuamua kurekodi wimbo maarufu duniani We Are the World.
SOMA: Buriani Tina Turner