Rais Mwinyi amuapisha Mwanasheria Mkuu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amemuapisha Dk. Mwinyi Talib Haji kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Hafla ya kuapishwa kwa Mwanasheria Mkuu huyo imefanyika Ikulu Zanzibar leo, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.

Dk. Mwinyi Talib Haji anachukua nafasi hiyo kwa lengo la kuendeleza juhudi za serikali katika kusimamia utawala wa sheria, ushauri wa kisheria kwa serikali pamoja na kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya kikatiba ya ofisi hiyo unaimarika.

Rais Mwinyi amempongeza Mwanasheria Mkuu huyo mpya kwa kuteuliwa kwake na kumtaka kutumia ujuzi na uzoefu wake kuhakikisha utawala wa sheria unadumishwa, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano na taasisi nyingine za serikali katika kukuza misingi ya haki na uwajibikaji.

 

 

 

 

 

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. Get more than £56,575,656,000 to help your society now via WhatsApp link

    I get to study PHD at Milembe University

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button