Mwandishi HabariLEO Mjumbe Mkutano Mkuu TFF

MWANDISHI wa michezo wa HabariLEO, Rahel Pallangyo amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanza nia (TFF) kutoka Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT).

Pallangyo alichagu liwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Tanga jana ambapo alimwangusha Allanus Lwena aliyekuwa anatetea nafasi yake.

Kwa upande wa Mwenyekiti, alichaguliwa Emanuel Chaula na wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa ni Maulid Mwikalo na Jovin Ndimbo.

Kadhalika Mwenyekiti Chaula alimteua Michael Kassanga kuwa Makamu Mwenyekiti kwani katiba inamtaka kuteua wajumbe watano watakaoingia kwenye Kamati ya Utendaji.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili George Banoba aliwataka viongozi wapya kufanya kazi kulingana na katiba ya FRAT.

“Mliochaguliwa wote mmeapishwa kulinda katiba na miongozo ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), FRAT na TFF hivyo katekelezeni majukumu yenu,” alisema Banoba.

Naye Mwenyekiti, Chaula aliwashukuru wajumbe kwa kumchagua na kuwaahidi kuwatumikia.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button