Mwandishi TSN ang’ara tuzo za TEF/UNICEF

Mwandishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Vicky Kimaro ni miongoni mwa washindi 12 wa Tuzo za Umahiri wa Habari za Watoto zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Habari za Watoto UNICEF
Tuzo hizo zimetolewa leo Desemba 29,2022 jijini Dar es Salaam.
Vicky ambaye ni mwandishi wa Daily News Digital, amepata tuzo ya mwandishi Bora wa Habari za kina ‘Best Analytical Reportage Award ‘na kuzawadia tuzo, cheti na fedha taslimu.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Vicky anasema: “Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa kibali na kuwa miongoni mwa wateule, nawashukuru waandaaji, uongozi mzima wa TSN na timu nzima ya Dailynews Digital, tuzo hii ni chachu kwangu ya kufanya kazi kwa bidii kuibua na kuhabarisha ishu za watoto na kuleta matokeo chanya kwa jamii.”
Mbali na Vicky wengine waliopata tuzoa hizo za umahiri katika Uandishi wa Habari za Watoto nchini Tanzania ni Faraja Masinde kutoka Mtanzania Digital, Tumaini Msowoya(Mwananchi – Shamba fmi), Marco Maduhu (Nipashe), Aidan Mhando (Chanel Ten) na Anord Kairembo (Radio Kwizera).
Wengine ni Julieth Mkireri (Nipashe), Judith Ndibalema (Majira), Shua Ndereka (Mviwata Radio), Sabina Martine (Rungwe fM Mbeya), Anna Sombida (EATV) na Stansaus Lambet (Dar 24).
Mratibu wa tuzo hizo Neville Meena amesema huo ni mwendelezo wa kuhakikisha habari za watoto zinaendelea kuandikwa.
Makamu Mwenyekiti wa TEF, Bakari Machumu amewataka waandishi kuendelea kuandika habari za watoto.