Mwendokasi waua 17 wakipeleka maiti Kilimanjaro

WATU 17 wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha fuso na gari la abiria ambalo lilikuwa limebeba maiti likitokea Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro.

Ajali hiyo imetokea katika Barabara Kuu ya Segera – Bwiko, eneo la Magila Gerezani, wilayani Korogwe mkoani Tanga. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omar Mgumba amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 10:30 alfajiri.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ‘ni mwendokasi.” 

Advertisement

RC Mgumba ameeleza kuwa dereva wa fuso alishindwa kuchukua tahadhari wakati akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake.

Taarifa za awali zinasema majeruhi 10 wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Bombo na wengine wawili wamebaki katika Hospitali ya Korogwe kwa matibabu.