Mwenendo na Uhimilivu wa Deni la Serikali

SERIKALI imesema hadi Aprili 2025, deni la Serikali lilikuwa shs trilioni 107.70.

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema hayo wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2025/26.

Dk Nchemba amesema kati ya kiasi hicho, deni la nje ni shs trilioni 72.94 na deni la ndani ni shs trilioni 34.76.

Amesema tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Oktoba 2024 imeonesha kuwa deni ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.

Katika tathmini hiyo, viashiria vinaonesha kuwa kwa mwaka 2024/25: thamani ya sasa ya deni la Serikali kwa Pato la Taifa ni asilimia 40.3 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55.

Thamani ya sasa ya deni la nje kwa Pato la Taifa ni asilimia 23.6 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 40; na thamani ya sasa ya deni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 123.8 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 180.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button