Mwenge wa Uhuru kukagua miradi ya bil 32/- Geita

MWENGE wa Uhuru 2024 umepokelewa katika Mkoa wa Geita na kuanza mbio zake wilayani Chato kwa shughuli ya kukagua, kuzindua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ukiwa mkoani Geita, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa km 826.6 na kupitia jumla ya miradi 65 yenye thamani ya Sh bilioni 32.2 iliyojengwa kwa pesa za serikali kuu, halmashauri na michango ya wananchi.

Advertisement

Mwenge wa Uhuru umewasili mkoani Geita ukitokea mkoani Kagera na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela katika uwanja wa Shule ya Sekondari Bwongela iliyopo wilayani Chato.

SOMA: Mwenge wa Uhuru wakagua miradi ya Sh Bil 5 Iramba

Akizungumza baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru, Shigela amefafanua kuwa mwenge wa uhuru utaweka jiwe la Msingi katika Miradi 18, kuzindua Miradi 22 pamoja na kutembelea na kuona miradi 25.

Shigella amesema miradi hiyo inapatikana kwenye halmashauri sita zilizopo kwenye wilaya tano ndaniya huo na itagusa sekta za afya, elimu, maji pamoja na jumuiya mbalimbali za wapinga rushwa na mazingira.

Mkuu wa wilaya ya Chato, Loys Peter amesema Mwenge wa uhuru ndani ya wilaya hiyo utakimbizwa umbali wa km 145, kupitia miradi 10 yenye thamani ya jumla ya Sh bilioni 10.6.

/* */