Mwenyekiti Chadema ajiunga CCM

GEITA. Bukombe. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kata ya Bulega wilayani Bukombe mkoani Geita, Dotto Ngaga ametangaza kuachana na chama hicho kwa madai amekosa wanachama.

Ngaga ametangaza uamuzi wake mbele ya Naibu Waziri Mkuu, ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Mbunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Dotto Biteko katika mkutano wa hadhara Kata ya Bulega, ambao oia ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda.

Akizungumuza na HabariLEO, baada ya uamuzi huo, Nguga amesema tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, wanachama wengi wa Chadema ndani ya Kata ya Bulega wamehamia CCM, hivyo Chadema kukosa nguvu.

Advertisement

“Chama (cha Chadema) katika Kata ya Bulega kimekufa, kwa sababu hata mimi hapa nilipo nilikuwa nimebakia mimi na Katibu, sasa hivi utendaji wa Chama Cha Mapinduzi utendaji ni mzuri, yaani watu wanawajali sana,” amesema na kuongeza kuwa ndiyo sababu yay eye kujitoa Chadema na kuhamia CCM.

Amesema utendaji mzuri wa serikali ya CCM ikiongozwa na Rais Samia umefanya kero nyingi za Kata ya Bulega kutatuliwa na kufanya wao kama viongozi wa upindani ndani na nje ya Bukombe kukosa hoja za kisiasa.

“Kazi ya mama (Rais Samia) ni nzuri mno, hapo zamani kulikuwa na usumbufu kwenye utendaji maeneo ya vijijini, vitu vingi vilikuwa haviwekwi vizuri, lakini sasa hivi hata unapowasomea watu na wao wanaona.

“Huu ni utendaji mzuri sana unaonekana kwa macho, kuna majibu ya kuona wala siyo kuambiwa. Kumbe utendaji mzuri huwa inafikia sehemu hata familia ya mtu inaguswa, na wala hakuna sababu nyingine kabisa,” amesema.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *